Njinsi ya kupika ndizi nyama au machalari vitu vinavyo hitajika ni ndizi , nyama, kitunguu maji, nyanya, hoho, karoti,mafuta, chumvi sufuria.Kwanza kabisa unakatakata nyama yako unaitia kwenye sufuria na maji kidogo, na chumvi ili iweze kuchemka. Unamenya ndizi zako unazigawa mara mbili ukimaliza unaziosha unaandaa viungo vyako unaweka ndizi kiasi kwenye sufuria alafu unaweka nyanya,vitunguu,karoti,hoho,mafuta, chumvi kiasi na nyama unaweka ndizi zilizobakia na maji kidogo ili ndizi ziweze kuiwa kwa utaratibu unafinika alafu unainjika jikoni unaweka moto wa saizi ziweze kuiva vizuri .Zikishakaribia kulainika unaongeza maji ya saizi ya mchuzi unaotaka nafinika zipate kuchempa unaepua.Na ndizi zako zitakuwa tayari unaweza kula na parachichi
Comments
Post a Comment