Skip to main content

 

Njinsi ya kupika ndizi nyama au machalari

 vitu vinavyo hitajika ni ndizi , nyama, kitunguu maji, nyanya, hoho, karoti,mafuta, chumvi sufuria.Kwanza kabisa unakatakata nyama yako unaitia kwenye sufuria na maji kidogo, na chumvi ili iweze kuchemka. Unamenya ndizi zako unazigawa mara mbili ukimaliza unaziosha unaandaa viungo vyako unaweka ndizi kiasi kwenye sufuria alafu unaweka nyanya,vitunguu,karoti,hoho,mafuta,  chumvi kiasi na nyama unaweka ndizi  zilizobakia na maji kidogo ili ndizi ziweze kuiwa kwa utaratibu  unafinika alafu unainjika jikoni unaweka moto wa saizi ziweze kuiva vizuri .Zikishakaribia kulainika unaongeza maji ya saizi ya mchuzi unaotaka nafinika zipate kuchempa unaepua.Na ndizi zako zitakuwa tayari unaweza kula na parachichi

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Vyakula vya kichagga---mangararimu

1.Njinsi ya kupika mangararimu      Mahitaji yanayo hitajika ni mahindi makavu,marage magadi,chungu na maji.unachambua mahindi vizuri kisha unainjika chungu jikoni kikiwa na maji unaweka mahindi kwenye chungu .Apo unakuwa tayari ushaloweka magadi na maji na tayari yameshatulia vizuri unachukuwa magadi yako unayapima kiasi unachoona yatatona kabla ujaweka magadi hakikisha umejachuja vizuri ala unafunika chungu chako unachochelea moto mpaka yatakapo lainika mahindi .unachukuwa ndoo yenye maji unamimina mahindi unayaosha ukimaliza unaweka maharage unarudisha tena jikoni mpaka maharage yatakapoiva na hapo mangararimu yetu yatakuwa yameshaiva na tayari kwa kuliwa.Unaweza kula na chai au maziwa
  Ndizi choma     Una andaa ndizi zako unaweza ukazichoma ndizi zako na maganda au ukazimenya unakuwa tayari ushawasha moto jikoni kuna mkaa .Unaweka ndizi zako ambazo ulizozimenya kwenye mkaa ziweze kuiva na mkaa taratibu .Ndizi za kuchoma na maganda unaziweka chini ya mkaa zinaiva na majivu