Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2019
  Ndizi choma     Una andaa ndizi zako unaweza ukazichoma ndizi zako na maganda au ukazimenya unakuwa tayari ushawasha moto jikoni kuna mkaa .Unaweka ndizi zako ambazo ulizozimenya kwenye mkaa ziweze kuiva na mkaa taratibu .Ndizi za kuchoma na maganda unaziweka chini ya mkaa zinaiva na majivu
Njinsi ya kupika kitawa.      Mahitaji ni ndizi, maziwa mtindi na magadi.Unamenya ndizi unazigawanya vipande vidogo vidogo unaziosha unaweka kwenye surufia unaweka maji kidogo na magadi kidogo unainjika jikoni unafinika zikishaiva unaepua na kuzisonga mpaka zilainike kabisa unaweka maziwa unaana ukupekecha na mpekecheo taratibu taratibu mpaka maziwa yajichanganye na ndizi na chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa.Chakula hiki huliwa sana na wazazi
  Njinsi ya kupika ndizi nyama au machalari   vitu vinavyo hitajika ni ndizi , nyama, kitunguu maji, nyanya, hoho, karoti,mafuta, chumvi sufuria.Kwanza kabisa unakatakata nyama yako unaitia kwenye sufuria na maji kidogo, na chumvi ili iweze kuchemka. Unamenya ndizi zako unazigawa mara mbili ukimaliza unaziosha unaandaa viungo vyako unaweka ndizi kiasi kwenye sufuria alafu unaweka nyanya,vitunguu,karoti,hoho,mafuta,  chumvi kiasi na nyama unaweka ndizi  zilizobakia na maji kidogo ili ndizi ziweze kuiwa kwa utaratibu  unafinika alafu unainjika jikoni unaweka moto wa saizi ziweze kuiva vizuri .Zikishakaribia kulainika unaongeza maji ya saizi ya mchuzi unaotaka nafinika zipate kuchempa unaepua.Na ndizi zako zitakuwa tayari unaweza kula na parachichi
Njinsi ya kupika kiburu au uberere kwa kirombo      Vitu vinavyohitajika ni maharage , ndizi, chungu, maji na magadi.Kwanza unaloweka magadi na maji ili yatulie vizuri kwa ajili ya kupikia kiburu.Unachambua maharage yako vizuri ukimaliza unayaosha unayaweka kwenye chungu unahinjika jikoni unachocholea moto mpaka yatakapo karibia kuiva .Maharage ya kiburu hayatakiwi kuiva sana baada ya hapo unakuwa tayari ushamenya ndizi .Ndizi unazitia kwenye chungu iliziweze kuiviana na maharage unaweka magadi kiasi ili viweze kuchemkiana unakaa kama dakika kumi hivi unaweka chumvi na mafuta ya kupikia unasubiri mpaka yaiviana kwenye chakula unaepua.Unasonga chakula chako vizuri ili viweze kuchanganyikana mpaka kilainike unaweka maji unaendekea kukichanganya na hapo chakula kipo tayari kwa kuliwa

Vyakula vya kichagga---mangararimu

1.Njinsi ya kupika mangararimu      Mahitaji yanayo hitajika ni mahindi makavu,marage magadi,chungu na maji.unachambua mahindi vizuri kisha unainjika chungu jikoni kikiwa na maji unaweka mahindi kwenye chungu .Apo unakuwa tayari ushaloweka magadi na maji na tayari yameshatulia vizuri unachukuwa magadi yako unayapima kiasi unachoona yatatona kabla ujaweka magadi hakikisha umejachuja vizuri ala unafunika chungu chako unachochelea moto mpaka yatakapo lainika mahindi .unachukuwa ndoo yenye maji unamimina mahindi unayaosha ukimaliza unaweka maharage unarudisha tena jikoni mpaka maharage yatakapoiva na hapo mangararimu yetu yatakuwa yameshaiva na tayari kwa kuliwa.Unaweza kula na chai au maziwa